Σάββατο 22 Ιουλίου 2017

Mtakatifu Moses wa Ethiopia († 405) – 28 Agosti



Musa Mwafrika, maarufu pia kama Musa Mwizi (330–405), alikuwa mmonaki padri nchini Misri na mmojawapo kati ya mababu wa jangwani.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 1 Julai na tarehe 28 Agosti.
Mzaliwa wa Ethiopia, Musa alikuwa mtumishi wa afisa wa serikali nchini Misri mpaka alipofukuzwa kwa thuhuma za kuiba na kuua.
Akiwa jitu, akawa bosi wa kundi la majambazi lililotisha watu wa bonde la Nile kwa ukatili.
Alipojaribu kukwepa waliokuwa wanamwinda, alifichama kwa wamonaki wa jangwani huko Wadi El Natrun (Sketes), karibu na Alexandria. Juhudi za kiroho, utulivu na furaha walivyokuwa navyo vilimuathiri kwa dhati. Muda mfupi baadaye aliacha mtindo wake wa kuishi, akabatizwa na kujiunga na monasteri ile.

Kwanza alipata shida sana kuzoea nidhamu ya jumuia ile. Alipovamiwa na wezi chumbani mwake, aliwazidi nguvu akawaburuza hadi katika kikanisa walimokuwemo wenzake wakisali ili aambiwe awafanyie nini wageni hao.
Musa alikuwa na ari katika yote aliyoyafanya, lakini alikata tamaa alipojitambua si mkamilifu kutosha. Hapo abati Isidori alimchukua alfajiri hadi juu ya paa ili kutazama miali ya kwanza ya jua. Halafu akamuambia, “Taratibu tu miali ya jua inaondoa usiku na kuleta mchana mpya, na vilevile taratibu tu mtu anakuwa mwanasala kamili.”
Baadaye Musa akawa mwenyewe kiongozi wa jumuia ya wakaapweke katika sehemu nyingine ya jangwa akapewa upadrisho.
Alipokuwa na umri wa miaka 75 hivi, ilisikika kwamba kundi la Waberber limepanga kushambulia monasteri yao. Wenzake walitaka kujihami, lakini Musa aliwazuia akawaambia ni afadhali wakimbie kuliko kushika silaha. Mwenyewe na wengine 7 walibaki hadi walipouawa tarehe 1 Julai.
Kwa sababu hiyo Musa Mwafrika anaheshimiwa leo kama mtetezi wa msimamo wa kukataa silaha katika kudai haki.

Source: Wikipedia

Icon of st Moses the Ethiopian 
by Julia Hayes, South Africa

Ona pia

Moses the Ethiopian, the Black Saint & Teacher (& other Ethiopian saints in the Orthodox Church)   
St MOÏSE L'ÉTHIOPIEN (ou "Le Noir" ou "Le Fort") et... Shawn "Thunder" Wallace
Brotherhood of St. Moses the Black

Watakatifu
 
Ancient Christian faith (Orthodox Church) in Africa 
The Orthodox Church of Alexandria & the Patriarchate of Alexandria  

The holy anarchists... in the Egyptian Desert 
"Oriental Orthodox"
 

St Moses the Ethiopian, 
Greek Orthodox holy icon

Δεν υπάρχουν σχόλια:

Δημοσίευση σχολίου