Παρασκευή 23 Ιουνίου 2017

Ndoa, Mitara na Kanisa la Orthodox


 
Ndoa ya Waorthodoksi Tanzania (kutoka hapa)

Sw.wikipedia
 
Kiongozi wa kabila la Toba 
na wake zake, 1892.
Mitara (au Upoli au Upali) ni hali ya watu zaidi ya wawili kuishi katika uhusiano wa kindoa.
Hali hiyo ilikuwa ya kawaida barani Afrika, ambapo mwanamume mmoja aliweza kuwa na wanawake zaidi ya mmoja, lakini kwa sasa inazidi kupungua.
Ya nadra zaidi ni hali ya wanaume kadhaa kuchanga mwanamke mmoja.
Baadhi ya nchi zinakubali hali hiyo, lakini nyingi zinaikataza.
Vilevile baadhi ya dini zinakubali mitara, hususan Uislamu, lakini nyingine zinaikataza, hususan Ukristo.
Katika Biblia tunakuta maendeleo ya ufunuo kuhusu hali hiyo kati ya Agano la Kale na Agano Jipya. 

Marejeo hapa.

Ndoa ya Wakristo ("kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa")

Sw.wikipedia / Ndoa (sakramenti)
 
“Siku ya tatu palikuwa na arusi huko Kana, mji wa Galilaya; naye mama yake Yesu alikuwepo. Yesu naye alikuwa amealikwa arusini pamoja na wanafunzi wake” (Picha kutoka hapa)

Ndoa kati ya wabatizwa wawili inahesabiwa na Kanisa Katoliki na Waorthodoksi kama mojawapo kati ya sakramenti saba zilizowekwa na Yesu Kristo.


Pamoja na Daraja takatifu ni kati ya sakramenti mbili za kuhudumia ushirika.

Fumbo la ndoa

Kadiri ya mpango wa Muumba, ndoa halisi ina sifa tatu: umoja, uimara na utayari wa kuzaa. “Hamkusoma ya kwamba yeye aliyewaumba mwanzo, aliwaumba mtu mume na mtu mke, akasema, ‘Kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe, na hao wawili watakuwa mwili mmoja?’ Hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi aliowaunganisha Mungu, mwanadamu asiwatenganishe” (Injili ya Mathayo 19:4-6). “Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, ‘Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha’” (Mwanzo 1:28). Mitara, uzinifu, talaka, ushoga na kukataa uzazi ni kinyume cha mpango huo.
Muungano usiovunjika mpaka kufa kati ya mwanamume mmoja na mwanamke mmoja waliobatizwa, ambao unafanyika kwa makubaliano yao ya hiari ambayo yanathibitishwa na Mungu anayewatia neema zinazohitajika waweze kutimiza malengo ya ndoa, ni ishara ya muungano wa kiarusi wa Yesu na Kanisa.
Yesu aliweka sakramenti ya ndoa kwa sababu ya umuhimu wa familia kwa ustawi wa mume na mke, watoto, jamii na ufalme wa Mungu, na kwa sababu ya uzito wa majukumu yanayohusika. “Siku ya tatu palikuwa na arusi huko Kana, mji wa Galilaya; naye mama yake Yesu alikuwepo. Yesu naye alikuwa amealikwa arusini pamoja na wanafunzi wake” (Injili ya Yohane 2:1-2), akaleta divai bora ya ndoa sakramenti badala ya ndoa ya kimaumbile. Hivyo ametuandalia neema tuweze kushinda “ugumu wa mioyo” (Mathayo 19:8) unaohatarisha daima uzuri wa mpango wa Mungu kuhusu upendo mwaminifu katika ndoa. “Mungu aliona kila kitu alichokifanya, na tazama, ni chema sana” (Mwanzo 1:31).




Ndoa ya Waorthodoksi Bujumbura (kutoka hapa)

Adhimisho la sakramenti ya ndoa

Ndoa ya Wakristo ni sakramenti ya Yesu na Kanisa lake. “Njoo huku, nami nitakuonyesha yule Bibi arusi, mke wa Mwanakondoo” (Ufu 21:9). Wakiwa na ndoa halisi, mume na mke waliobatizwa ni ishara wazi ya hao wanaarusi wawili wasioonekana. “Kama vile Kanisa limtiivyo Kristo, vivyo hivyo wake nao wawatii waume zao katika kila jambo. Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake” (Ef 5:24-25). Ndiyo sababu Mkatoliki hawezi kufunga ndoa bila ya kuhusisha Kanisa na kufuata taratibu zake.
Kwa kawaida Wakatoliki wanaiadhimisha wakati wa Misa, karamu ya arusi ya Mwanakondoo na Kanisa, lakini wanakubali katika mazingira ya pekee iweze kufungwa na wanaarusi mbele ya mashahidi wawili hata bila ya kuwepo padri .
Kumbe Waorthodoksi wanahesabu baraka ya padri kuwa sehemu ya lazima ya sakramenti, ambayo wanaarusi wanapewa.

Kubariki ndoa kwa Waprotestanti

Martin Luther aliona sakramenti sharti iwe alama iliyowekwa na Yesu Kristo mwenyewe, lakini ndoa ni sehemu ya utaratibu wa uumbaji uliotangulia kuja kwa Yesu.
Kwa sababu hiyohiyo Waprotestanti wengi hawakubali ndoa kuwa sakramenti na wanabariki tu ndoa iliyofungwa kufuatana na sheria za dola.


Ndoa ya Waorthodoksi Madagascar (kutoka hapa)
 
Tunaelewa kuwa mtu wa Kiafrika na wake wengi anaweza kuwapenda wote. Tunaheshimu hii. Lakini katika Agano la Kale, Mungu aliumba jozi la kwanza la watu, mtu mmoja na mwanamke mmoja tu, Adamu na Hawa. Hii inathibitisha kwamba mwanamume na mwanamke ni wa thamani sawa. Pia inathibitisha kuwa ndoa pekee ambayo Mungu anapenda kweli, ni ndoa kati ya mtu mmoja na mwanamke mmoja.
Kwa hiyo, katika Kanisa la Orthodox, ambalo anakupenda mwanadamu (mwanamume na mwanamke) sana, mitara haiwezi kukubalika.




Bibi na arusi wakati wa harusi Waorthodoksi (hapa)
Ona pia

Polygamy in Africa and Orthodox Church
Orthodox Women Saints (picha)
Orthodoxes chrétiens Mariages en Afrique 
Which One Should I Deny? / "Leave, you who loves him more..." - A True Story from the Years of the Missionary Fr. Cosmas Grigoriatis
Theotokos

Wanawake wa Afrika 
Femmes Africaines

African Women

Male and Female Created He Them  
Wakristo Orthodox ya Afrika 
Kanisa la Orthodox na Kanisa Katoliki  
KUTAFUTA IMANI LAKUNYOLOKA – AMA KI ORTHODOKSI  

 Ndoa ya Waorthodoksi Pwani ya Pembe (kutoka hapa - video hapa)

Δεν υπάρχουν σχόλια:

Δημοσίευση σχολίου