Δευτέρα 2 Νοεμβρίου 2015

Mt. Yohane wa Dameski na picha ya Bikira na Tatu Mikono


Nakala hii ina taarifa kutoka humo : Sw.wikipedia na maneno yangu mwenyewe

Yohane wa Dameski (kwa Kiarabu يوحنا ابن ﺳﺮﺟﻮﻥ Yuḥannā ibn Sarjūn) alikuwa mmonaki, padri na mwanateolojia kutoka Dameski mji mkuu wa Siria (Damasko, 676? - Palestina, 749?).

Tangu zamani anaheshimiwa kama mtakatifu na babu wa Kanisa.

Ni msimamizi wa wachoraji.

Sikukuu yake inaadhimishwa kila mwaka tarehe 4 Desemba.

Maisha

Alizaliwa Damasko mwaka 676 hivi, labda katika familia ya Kiarabu ya Kikristo. Baba yake alikuwa Sarjūn ibn Manṣūr. Babu yake, Manṣūr, alikuwa wa kwanza katika familia kupewa vyeo vikubwa chini ya utawala wa halifa Mu'awiya bin Abi Sufyan na wa waandamizi wake.

Baba yake pia alikuwa mwanasheria, akafuatwa na Yohane ambaye bado kijana alipata kuwa mshauri wa halifa wa Damasko na msimamizi wa mali yake.

Lakini baadaye kidogo huenda akahukumiwa na kukatwa mkono wa kushoto. Hapo (mwaka 700 hivi) alihama mji huo na kujiunga moja kwa moja na monasteri ya Mt. Saba, kati ya Bethlehemu na Yerusalemu, ambapo alipewa upadrisho.

Alihubiri na kuandika sana hadi kifo kilipompata huko Palestina akiwa na umri wa miaka 73 (mwaka 749 hivi).

Katika maandishi yake alikusanya mafundisho ya mababu waliomtangulia.

Kitabu chake maarufu zaidi kinaitwa Kuhusu Imani Sahihi. Pia ametuachia tenzi bora kwa ajili ya liturujia.

Alitumia nguvu zake zote hasa kutetea matumizi ya picha na sanamu takatifu katika Ukristo dhidi ya waliotaka kuziteketezakwa kushikilia makatazo ya Agano la Kale, lakini pia kwa kujilinganisha na Uislamu kwa malengo ya kisiasa.
 

Bikira Maria kuponywa mkono severed ya Mt. Yohane wa Dameski.
Kisha Saint John umba picha ya Bikira na Tatu Mikono, kukwama fedha mkono kuwashukuru Bikira Maria. Kusoma zaidi hapa (kwa Kiingereza).


Hoja zake zilitegemea hasa umwilisho wa Mwana wa Mungu tumboni mwa Bikira Maria. “Zamani Mungu, akiwa hana mwili wala sura, hakuchorwa kwa picha. Lakini, kwa kuwa sasa ameonekana katika mwili na kuishi kati ya watu, mimi nachora upande ule wa Mungu ulioonekana. Siabudu maada, bali Muumba wa maada ambaye alipata kuwa maada kwa ajili yangu, akakubali kuishi katika maada na kuniokoa kwa njia ya maada. Kwa hiyo sitaacha kuheshimu maada ile ambayo wokovu wangu umepatikana kwa njia yake. Ila siiheshimu kikamilifu kama Mungu! Ingewezaje kuwa Mungu kile kilichopewa kuwepo kutoka utovu wa vyote?.… Hata hivyo mimi naheshimu na kustahi pia maada nyingine yote iliyoniletea wokovu, kwa kuwa imejaa nguvu na neema takatifu. Je, mbao za msalaba uliobarikiwa mara tatu si maada?… Na je, wino, na kitabu kitakatifu sana cha Injili, si maada? Je, altare ya ukombozi inayotupatia Mkate wa uzima si maada?… Na, muhimu kuliko yote, je, mwili na damu ya Bwana wetu si maada? Basi, ama tunatakiwa kufuta umbile takatifu la vitu hivyo vyote, ama tunatakiwa kulikubalia mapokeo ya Kanisa heshima ya picha za Mungu na za marafiki wake ambao wametakaswa na jina walilopewa, na kwa sababu hiyo wanatawaliwa na neema ya Roho Mtakatifu. Basi, usiikosee maada: haitakiwi kudharauliwa, kwa sababu hakuna kilichofanywa na Mungu ambacho ni cha kudharauliwa”.

Hivyo Yohane alikuwa kati ya wale wa kwanza waliotofautisha ibada inayotupasa kwa Mungu tu na heshima inayoweza kutolewa kwa malaika na watakatifu wake na hata kwa picha zinazowachora, ambayo imestawi hasa katika Makanisa ya Mashariki hadi leo. Kwa jumla ni mtazamo mpya, chanya, juu ya ulimwengu: maada yenyewe inaweza kufanywa chombo cha neema kwa kuitiwa Roho Mtakatifu.

Alipewa ushindi na Mtaguso wa pili wa Nisea (787) baada ya kifo chake.

Sala yake

Wewe, Bwana, ulinitoa katika viuno vya baba yangu; wewe uliniunda tumboni mwa mama yangu; wewe ulinitoa mwangani, mtoto uchi, kwa kuwa sheria za umbile letu zinafuata daima amri zako.

Wewe uliandaa kwa baraka ya Roho Mtakatifu uumbaji wangu na maisha yangu, si kadiri ya matakwa ya mtu wala ya tamaa ya mwili, bali kadiri ya neema yako isiyosemeka.

Uliandaa uzazi wangu kwa matayarisho yanayopita sheria za umbile letu, ulinitoa mwangani kwa kunifanya mwanao, uliniandika kati ya wafuasi wa Kanisa lako takatifu lisilo na doa.

Umenilisha maziwa ya Kiroho, maziwa ya maneno yako ya Kimungu.

Umenitegemeza kwa chakula kizito cha Mwili wa Yesu Kristo, Mungu wetu, Mwanao pekee mtakatifu sana, umenilevya kwa kikombe cha Kimungu cha Damu yake itiayo uzima, aliyoimwaga kwa wokovu wa ulimwengu wote…

Sasa, Bwana, kwa njia ya kuhani wako umeniita nitumikie wanafunzi wako.

Sijui kwa mpango gani umefanya hivi; wewe tu unajua…

Unichunge, Bwana, na uchunge mwenyewe pamoja nami watu wengine, ili moyo wangu usiniinamishe kulia wala kushoto, bali Roho wako mwema unielekeze njia nyofu ili matendo yangu yafuate matakwa yako, na yayafuate kweli mpaka mwisho.

Vyanzo

Viungo vya nje

[1] Maandishi yake yote pamoja na faharasa katika Patrologia Graeca ya Migne
"Apologia Against Those Who Decry Holy Images" at the Internet Medieval Sourcebook
A Philosophical Explanation of Hypostatical Union in John Damascene's Fount of Knowledge
The Concept of Unbounded and Evil Matter in Plotinus and John Damascenus
Works by John of Damascus katika Project Gutenberg
"St. John of Damascus' Critique of Islam" at the Orthodox Christian Information Center
Greek Opera Omnia by Migne, Patrologia Graeca with Alaytical Indexes
St John of Damascus Orthodox Icon and Synaxarion (4 Desemba)


Ona pia

Picha takatifu katika Kanisa la Orthodox 
Yesu Kristo - Mungu akawa mtu na mtu inakuwa kama mungu
Utatu Mtakatifu, Mungu ambaye anapenda ubinadamu

Bikira Maria, Mama wa Mungu
Kanisa la Orthodox na Kanisa Katoliki
 
Katika mwanga wa Mungu
Historia ya Kanisa la Orthodox : Ukristo barani Afrika

Maaskofu Orthodox watakatifu watatu: Basili Mkuu, Yohane Krisostomo na Gregori wa Nazianzo

Δεν υπάρχουν σχόλια:

Δημοσίευση σχολίου